Azam FC imetinga Fainali ya Kagame cup baada ya kuifunga AS Vita ya DRC 2-1, shukrani kwa magoli ya John Bocco JB19 na Mrisho Ngasa MG16…. tunasubiri mshindi kati ya Yanga na APR

Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry

http://bongostaz.blogspot.com/2012/07/azam-watangulia-fainali-ngassa.html

 

Goli la ushindi la mchezaji Mrisho Ngassa wa Azam FC, limeivusha timu hiyo na kuingia fainali ya Kombe la Kagame 2012 kwa kuifunga AS Vita Club 2-1, Azam sasa itacheza na Yanga kwenye mchezo utakaopigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Azam FC imeshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza imeingia moja kwa moja fainali ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Katika mchezo wa nusu fainali Azam FC imeifunga AS Vita Club ya Congo DRC 2-1 na kufanikiwa kuingia fainali ambapo watacheza na Yanga ambayo imeibuka mshindi kwa kuifunga APR ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa jioni.

Wachezaji wa Azam FC kwa umoja wao wakiwa na nia ya kufika fainali walianza mchezo huo kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi kipindi cha kwanza lakini hayakuzaa matunda.

Kiungo Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ kama ilivyo kawaida yake alikua kiongozi wa timu kwa kuwatengenezea washambulia nafasi huku nahodha Agrey Morris akisimamia vyema safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Katika mchezo huo Vita walikuwa wa kwanza kupata goli katika dk 34 lililowekwa wavuni na mchezaji Mfongang Alfred, goli lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko alitoka Jabir Aziz nafasi yake ikachukuliwa vema na Mrisho Ngassa, mabadiliko hayo yaliimarisha safu ya ushambuliaji ya Azam FC na kupelekea mshambuliaji John Bocco kusawazisha bao hilo kwa kichwa akimalizia krosi ya Erasto Nyoni na kufaya matokeo kuwa 1-1.

Goli hilo la kusawazisha liliamsha kasi kwa Azam FC ambapo walifanya mabadiliko tena alitoka beki Ibrahim Shikanda akaingia Samir Haji Nuhu na dakika ya 82 alitoka Tchetche Kipre nafasi yake ikachukuliwa na Gaudece Mwaikimba.

Kuingia kwa wachezaji hao Azam FC walianza kufanya mashambulizi ya kasi kwa kufika langoni kwa Vita mara kwa mara, dakika moja kabla mchezo kumalizika, Mrisho Ngassa aliwainua mashabiki wa Azam FC kwa kupachika goli la pili na la ushindi baada ya kupiga shuti lilitinga moja kwa moja wavuni, na kumalizika mchezo Azam FC wakiwa kifua mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Vita Club.

Katika mchezo huo mwamuzi Dennis Bate wa Uganda dk 41 alimtoa kwa kadi nyekundu mchezaji wa Vita, Issama Mpeko baada ya kumuonya kwa kadi mbili za njano.

Bocco amefikisha magoli matano katika mashidano  hayo akiwa ni mmoja wa wachezaji wanaowania kiatu cha dhahabu endapo atapata magoli mawili katika mchezo wake wa fainali ili kuwazidi wachezaji Taddy Etekiama wa AS Vita mwenye magoli sita na Hamis Kiiza na Said Bahanuzi wa Yanga wenye magoli matano kila mmoja.

Azam FC Deogratius Munishi, Ibrahim Shikanda/Samir Haji Nuhu, Erasto Nyoni, Said Morad, Aggrey Moris, Jabir Aziz/ Mrisho Ngassa 45’, Kipre Tchetche/ Gaudence Mwaikimba 82’, Salum Aboubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

AS Vita Club, Lukong Nelson, Ilongo Ilifo, Issama Mpeko red card 41’,Ebunga Simbi, Mapuya Lema, Mfongang Alfred, Niemba Nkanu, Magola Mapanda, Mutombo Kazadi, Lema Mubidi na  Etekiama Taddy.