Ikishiriki kwa mara ya kwanza Kombe la Kagame timu ya Azam FC imetinga nusu fainali kwa kuichapa Simba SC 3-1 huku mshambuliaji John Bocco akifunga mabao yote matatu ‘hat-trick’.

Azam FC imecheza mchezo huo wa robo fainali na kuwashangaza mashabiki wa soka nchini kwa kupata ushindi mzito ulioivusha timu hiyo hadi nusu fainali ya mashindano hayo ambapo watakutana na AS Vita Club ya Congo DRC katika mchezo huo wa nusu fainali utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Maandalizi mazuri ya Azam FC yaliwafanya kutawala mchezo huo vipindi vyote viwili na kufanya mashambulizi mara kwa mara.

Azam FC sehemu ya kiungo ilioekana kuwa vuzuri kuliko Simba, mchezaji Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ alitengeneza nafasi na kuchezesha timu katika kiwango cha juu akitoa pasi kwa washambuliaji wake kupelekea kupatikana kwa mabao hayo.

Bocco alianza kwa kupachika bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya 17 ya mchezo huo akimalizia krosi ya mwisho iliyopigwa na mchezaji Khamis Mcha Viali.

Bao hilo liliwapa kasi Azam FC katika kipindi cha kwanza na kuongeza kasi ya mashambulizi, katika dk 12 Azam FC walifanya mabadiliko ya kwanza ambapo kiungo Michael Balou Kipre alitoka baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo nafasi yake ikachukuliwa vema na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ aliyeongeza radha ya mchezo huo.

Timu zilienda mapumziko Azam FC ikiongoza kwa 1-0, Kipindi cha pili kilianza timu zilirudi kama zilivyo, dk ya 46 Bocco akatumia uzembe wa beki ya Simba na kuachia shuti lililomshida kipa wa Simba Juma Kaseja na kuandika bao la pili kwa Azam FC.

 

Kupatikana kwa bao hili ikawa chachu ya mashambulizi kwa timu zote, dk ya 53 Simba walipata bao lao pekee lililofungwa na beki Shomari Kapombe.

 Azam FC walifanya mabadiliko dk 60 alitoka Kipre Tchetche nafasi yake ikachukuliwa na George Odhimbo ‘Blackberry’ na dk 70 Jabir Aziz aliingia kuchukua nafasi ya Khamis Mcha, mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kuongeza kasi ya mashambulizi.

Kadri muda ulivyozidi kwenda Azam FC wakaongeza nguvu ya mashamulizi kwa kufika langoni mwa Simba mara kwa mara na kuifanya timu hiyo kucheza mchezo wa nguvu zaidi, dk ya 73 Bocco alijihakikishia nafasi ya kuondoka na mpira wake baada ya kuandika bao la tatu akicheza vizuri na Jabir Aziz na kumtungua kipa Kaseja na kumuacha kipa huyo asiamini macho yake.

Goli hilo la tatu na la mwisho katika mchezo huo liliituliza Azam FC na kuanza kucheza soka kwa kugongeana pasi nyingi wakiwaacha Simba wanahangaika huku muda ukizidi kwenda.

Kwa matokeo hayo Azam FC imeitoa Simba katika michuano hiyo, itakutana na AS Vita Club ya Congo ambayo imeingia nusu fainali baada ya kuifunga 2-2 timu ya Atletico ya Burundi, mchezo huo wa nusu fainali utachezwa siku ya Alhamisi.

Azam FC waliong’aa siku ya leo kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki Ibrahim Shikanda, Agrey Moris, Erasto Nyoni na Said Morad, viungo Michael Bolou/Ramadhan Chombo 12’, Salum Aboubakar, Khamis Mcha/Jabir Aziz 70’ washambuliaji Tchetche Kipre/George Odhiambo 60’ na Joh Bocco.

Mwisho

 

Stewart:

Baada ya kupata ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Simba, kocha wa Azam FC Stewart Hall ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wake na kumpongeza John Bocco kwa kufunga mabao yote matatu ‘hat-trick’.

Ushindi huo umeivusha Azam FC na kuingia hatua ya nusu fainali ya amshindano ya Kombe la Kagame 20120 yanayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stewart alisema ushindi huo umetokana na juhudi za wachezaji wake, maandalizi mazuri na kufuata maelekezo yake.

“Wamefanya tulichowatuma, niliwataka wacheze mpira na kufunga magoli, wamenifurahisha kwa kufata maagizo, nimeridhishwa na kiwango walichoonyesha kwenye mchezo wa leo” alisema Stewart.

Stewart aliongeza kuwa wanaelekeza macho yao katika mchezo wa nusu fainali ili wapate ushndi utakaowawezesha kucheza fainali ya kombe hilo wakiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Kocha huyo alimpongeza mshambuliaji wake John Bocco kwa kufunga mabao yote matatu, akiyaita magoli ya ufundi na magoli mzuri.

Amesema juhudi binafsi za mchezaji huyo kwa kutumia uwanja wao wa mazoezi ulioko Chamazi, ameweza kuongeza uwezo wake kwa kufunga magoli mazuri na katika umbali wowote.

“Ni juhudi zake kutokana na mazoezi anayofanya kila siku, amerekebisha makosa yake na sasa anafanya vizuri nampongeza na namtaka aongeze bidii” alisema Stewart.