Kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema timu yake itapambana kadri ya uwezo wake kuhakikisha inavuka na kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Kagame 2012.

Azam FC, kesho Jumamosi itacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Tusker ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tusker katika mchezo wake wa kwanza ilitoka suluhu na Mafunzo, hivyo Mafunzo kuwa na pointi mbili baada kutoka sare ya 1-1 na Azam FC.

Katika kundi hilo B, Mafunzo inaongoza kwa kuwa na pointi 2 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi moja baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mafunzo, Tusker nao wana pointi moja, hivyo mchezo kati ya Azam FC na Tusker utatoa majibu ya timu zitakazoingia robo fainali ya mashindano hayo.

Akizungumzia mchezo huo ambao Azam FC inatakiwa kushinda ama kutoka sare iweze kupita, kocha Stewart alisema amewaandaa wachezaji wake kukabiliana na mchezo huo mgumu na wenye kulete sura mpya ya timu yake ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo yanayokutanisha vilabu kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Alisema timu imejipanga vizuri, wachezaji nao wapo katika hari nzuri ya kutafuta kuvuka hatua ya makundi.

“Naamini kwa maandalizi tuliyofanya tutashinda katika mchezo huo, japo mpira una matokeo tofauti lakini lengo letu na kushinda” alisisitiza Stewart.

Aliongeza kuwa matokeo ya sare kwa timu za kundi hilo, yanatoa urahisi kwao na pia yanaweza kuleta mabadiliko katika mchezo wa mwisho hivyo timu yake inatakiwa kushinda na sio kutegemea sare yoyote.

1.. Deogratius Munishi Dida (27)

2. Ibrahim Shikanda (21)

3. Erasto Nyoni (6)

4. Aggrey Morris (13)

5. Joseph Owino (12)

6. Kipre Bolou (29)

7. Kipre tchetche (10)

8. Ibrahim Mwaipopo (4)

9. John Raphael Bocco (19)

10. Ramadhan Chombo (17)

11. Khamis Mcha Khamis (22)