Azam FC leo inaingia uwanjani kuweka historia mpya kwa kukwaana na timu ya Mafunzo ya Zanzibar katika mashindano ya CECAFA Kagame Cup
Ni historia mpya kwa klabu kutokana na ukweli kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kushiriki mashindano makubwa kama haya.
Kocha Stewart Hall amekwisha weka bayana kikosi kitakachoanza leo ambapo golikipa mpya Deogratius Munishi Dida ndiye atakayesimama langoni huku Erasto Nyoni akicheza beki wa kulia.
Waziri Salum leo atarudi uwanjani na kucheza beki wa kushoto na mchezaji bora nchini Aggrey Morris atasimama katikati akishirikiana na Joseph Owino Gere.

Viungo watatu watakuwa ni Kipre Bolou, Salum Abubakar na Ramadhan Chombo Redondo wakati mfungaji bora wa klabu John Raphael Bocco atasimama katika ushambuliaji akishirikiana na Kipre Tchetche na Mrisho Ngasa.
Endapo Azam FC itashinda kwa idadi kubwa ya magoli basi itakuwa imejihakikishia nafasi kwenye robo fainali. Timu nyingine kwenye kundi hili ni Tusker ya Kenya ambayo itakwaana na Azam FC wikiendi ijayo.