Timu ya Azam FC leo itacheza mchezo wake wa nusu fainali ya mashindano ya Urafiki Tanzania dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Super Falcon kwenye uwanja wa Amaan visiwani hapa.

Azam FC imejiandaa kikamilifu kucheza mchezo huo na kupata ushindi ili wapate nafasi ya kucheza fainali za mashindano hayo zitakazofanyika siku ya Jumatano.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala alisema wameajiandaa vizuri kucheza mcheza mchezo huo kwa kuwa wachezaji wote wana hali nzuri.

Akizungumzia Super Falcon, Kali alisema timu hiyo ya kutoka Pemba haina tofauti na zingine kwa kuwa zinacheza mpira wa aina moja na wameshacheza na timu mbili hivyo hawatawapa shida.

“Sisi tupo vizuri, timu za huku zinafanana aina ya uchezaji huwa wanapigana hadi mwisho wa mchezo tumejiandaa kwa hilo lakini lolote linaweza kutokea huu ni mpira” alisema Kali.

Aliogeza kuwa mazingira ya uwanja ni changamoto kwa wachezaji wake kwa kuwa uwanja huo hauna kiwango kizuri kwa kuchezea