Azam FC jiuoni hii imeifunga Mafunzo ya Zanzibar 3-2 katika kinyang’anyiro cha Urafiki Cup, mashindano yanayoendelea visiwani Zanzibar

 

Magoli ya Azam FC jioni hii yalifungwa na Ramadhani Chombo, Kipre Tchetche na Ibrahim Mwaipopo

Kiujumla Azam FC iliutawala mchezo wa leo, kwa matokeo haya sasa Azam FC inasubiri matokeo ya mechi ya usiku huu kati ya Simba na Karume Boys mechi itakayoanza saa mbili usiku.

Kwa matokeo hayo Azam FC itakutana na Super Falcon kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza utakaochezwa siku ya Jumatatu jioni kwenye uwanja huo.

Katika mchezo huo Azam FC ilikuwa chini ya nahodha Mkenya Ibrahim Shikanda, ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa kiungo Ramadhan Chombo ‘Redondo’ aliyepiga mpira wa kona iliyoenda moja kwa moja wavuni ikisindikizwa na kipa wa Mafunzo Salum Pangani.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha kizuri kwa Azam FC walitawala mpira muda wote huku wakipata bao la pili katika dakika ya 37 lililofungwa na Tchetche Kipre akimalizia kazi nzuri ya Abdulhalim Humud.

Kipre amefikisha mabao mawili katika mashindano hayo baada ya kufunga katika mchezo wa juzi, huku wachezaji Odhiambo, Chombo na Mwaipopo wakiwa na goli moja moja.

Wakati magoli hayo yakiingia wavuni mchezaji wa Azam FC, George Odhiambo ‘Blackberry’ kwa nyakati tofauti alitengeneza nafasi nyingi lakini hakuweza kufunga.

Kipindi cha pili kilianza kwa Mafunzo kupata bao la kwanza katika dakika ya 46 kufuatia uzembe kiungo Abdulhalim Humud na kipa wa Azam FC, Deogratius Munishi ‘Dida’ Humud alirudisha kwa kipa mpira ambao ulimshinda kutokana na ubovu wa kiwanja na Dida alijaribu kutuliza mpira na kupata wakati mgumu kutokana na uwanja kuwa na mabonde na kumuacha mchezaji wa Mafunzo Mohamed Abdulrahman kuandika bao hilo.

Azam FC wakiwa wanatafakari kuruhusu bao hilo walifanya mabadiliko walitoka Michael Bolou Kipre, Geoge Odhiambo na Abdulhalim Humud na kuingia Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao na Khamis Mcha Viali mabadiliko yalibadili mchezo kwa kiasi kikubwa.

Mafunzo walitumia vyema uzembe wa kiungo wa Azam FC Abdulhalim Humud tena kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 69 kupitia kwa Jaku Joma na kufanya matokeo kuwa 2-2 kabla ya Mwaipopo kuifungia Azam FC bao la ushindi kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni kwa ustadi mkubwa katika dakika ya 83 na kumalizika mchezo kwa  Azam FC ikipata ushindi wa 3-2.

Katika mchezo mwingine wa mashindano hayo Simba SC nayo imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga 1-0, Zanzibar U-23, Simba itasubiri kucheza na mshindi wa mchezo wa leo kati ya Jamhuri na Zanzibar All Stars.

Azam FC Deo Munishi,  Samir Haji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Said Morad, Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Kipre Tchetche, Michael Kipre/Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Ramadhan Chombo na George Odhiambo.