Baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Simba, Azam FC imeelekeza nguvu katika mchezo wake wa mwisho leo dhidi ya Mafunzo ili wapate nafasi ya kuingia nusu fainali ya michuano ya Urafiki Tanzania inayoendeela kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Endapo Azam FC itashinda mchezo huo itaingia hatua ya nusu fainaili ya mashindano hayo, huku Mafunzo wao wakiwa wameshatolewa kwa kufungwa michezo miwili, Azam FC ina pointi mbili nyuma ya Simba na Zanzibar U23 zenye pointi 4 kila moja.

Endapo Azam FC itashinda kwa tofauti ya 2-0 basi itafuzu moja kwa moja bila kujali matokeo ya mechi kati ya Simba na Karume Boys

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amesema ni lazima washinda mchezo huo kwa kuwa wanahitaji kuingia nusu fainali na anaamini wachezaji wake wanaweza kukamilisha lengo hilo.

"Kwa sasa tunaangalia kushinda mchezo  huo ndio suala lililopo, nawaamini wachezaji wangu watashinda mchezo " alisema Kali.