Kocha msaidizi wa Azam FC, Kalli Ongala amesema kikosi chake kilichopo visiwani Zanzibar kipo tayari kupambana na Simba kwenye mchezo wa pili hatua ya makundi wa mashindano ya Urafiki Tanzania.

Azam FC ipo visiwani hapa kwenye mashindano ya Urafiki Tanzania, kesho itacheza na Simba kwenye Uwanja wa Amaan.

Kali alisema wachezaji wote wako tayari kucheza na timu yoyote kwa kuwa kikosi chake kina wachezaji mahiri na wenye uwezo wa kucheza na timu yoyote watakayokutana nayo.

Akizungumzia hali za wachezaji Kali alisema wachezaji wote wana hali nzuri isipokuwa kiungo Abdi Kassim hatoweza kucheza mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria na Jabir Aziz ambaye anaumwa macho.

Kali aliongeza kuwa mashindano hayo muhimu kwa wachezaji wake ambao wanajiandaa kucheza mashindano ya kimataifa ya kombe la Kagame na michezo ya ligi kuu msimu ujao.

Hii itakuwa mara ya ya tatu Simba na Azam kukutana katika michezo tofauti kwa mwaka huu, Kombe la Mapinduzi Azam FC iliifunga Simba 2-0 na kuwatoa kwenye mashindano hayo na kwenyeligi kuu Simba iliifunga Azam FC 2-0.