Kikosi cha Azam FC kesho kitalekea visiwani Zanzibar kushiriki mashindano ya Ujirani Mwema yatakayoanza kutimua vumbi kwenye viwanja vya Amaan visiwani humo.

Azam FC itaondoka bila ya wachezaji wake saba waliokuwa timu ya Taifa ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambao watabaki kujiandaa kwajili ya mechi za Kombe la Kagame litakaloanza Julai 14 mwaka huu.

Kocha wa Azam FC, Stewart Hall alisema wachezaji wengine hawatakwenda kwenye mashindano hayo kwa kuwa Kagame ni muhimu kuliko mashindano hayo ya Zanzibar.

Aliwataja wachezaji watakao kwenda kuwa ni Ibrahim Shikanda, Joseph Owino, Luckson Kakolaki, Ibrahim Mwaipopo, George Odhiambo, Abdulghan Gulam, Samir Haji Nuhu ,Jackson Wandwi, Said Morad, Abdulhalim Humud, Omary Mtaki, Himd Mao, KIpre Tchetche, Mwaikimba, Michael Kipre na Ramadhan Chombo 'Redondo.

Watakaobaki nay eye ni Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar na John Bocco