Kilikuwa ni kitu kisichotarajiwa baada ya timu ya Azam Academy kuweza kuonyesha ukomavu wao kwa kuwafunga kaka zao Azam FC, 3-2 kwenye mchezo wa kupimana nguvu uliochezwa uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Azam FC na Academy zinajiandaa na mashindano makubwa, Azam FC kesho wataelekea visiwani Zanzibar kushiriki kombe la ujirani mwema kabla ya kucheza Kombe la Kagame wiki mbili zijazo huku Academy wao wanajiandaa na mashindano ya vijana Afrika Mashariki ya Rolling Stone yatakayofanyika nchini Burundi.

Katika mchezo huo uliovuta hisia za wachezaji wa pande zote hasa baada ya siku ya Jumatano kucheza mchezo wa kwanza ambapo Azam FC wakishinda 2-1, kwa taabu Academy wameweza kulipa kisasi cha mabao hayo kwa kuwafunga ndugu zao 3-2.

Vijana wa Academy wakiongozwa na nahodha wao Abdul Mgaya wamepata ushindi huo ikiwa ni siku moja baada ya kuifunga timu ya JKT Ruvu 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye kambi ya JKT Mlalakuwa.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Zahor Pazi, bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha timu zote zilifanya mabadiliko, Azam FC ya wachezaji wote ingawa baadhi ya wachezaji walirudi tena uwanjani baadaye..

Kikosi cha kwanza cha Azam FC kilichopata ushindi wa 1-0 kilikuwa chini ya nahodha Ibrahim Shikanda, Joseph Owino, Luckson Kakolaki, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, George Odhiambo, Abdulghan Gulam, Samir Haji Nuhu, Hamis Mcha Viali na kipa Jackson Wandwi.

Mabadiliko hayo kwa Azam FC hayakuweza kuongeza magoli, dk ya 46 Said Moradi alisawazisha bao hilo kwa goli la Kujifunga akimalizia vyema pasi ya mwisho kutoka kwa Ahmed Abbas. Kujifunga kwa Moradi kulitokana na Kuzidiwa ujanja na Kevin Friday ambaye alimbada na kumfanya beki huyo mzoefu ajifunge.

Academy waliokuwa wanatawala mchezo lakini vipindi vyote walifanya makosa ambapo katika dk 65 walizubaa kuondosha mpira kwenye eneo la hatari na kupelekea Azam FC kupata bao la pili lililowekwa wavuni na mshambuliaji mwenye mwili mkubwa Gaudence Mwaikimba aliyetumia vyema krosi ya Kipre Tchetche na kufanya matokeo yakawa Azam FC 2-1 Academy.

Matokeo hayo hayakuididimiza Academy zaidi waliamka na kufanya mashambulizi mfululizo, dk 72 Kelvin Friday alichonga mpira uliompita kipa wa Azam FC, Wandwi baada ya kutumia vizuri kosa la beki Said Morad aliyetaka kuucontrol mpira wa juu ambao ulimshinda na kumpa nafasi Kevin na kuandika bao hilo la kusawazisha.

Kevin Friday leo alitawala eneo la mbele na Azam Academy na aliwapa tabu sana walizi wa timu ya wakubwa ambapo katika dakika ya 80, aliwapunguza mabeki wa timu ya wakubwa akiwemo Moradi na kutoa pasi nzuri kwa Jamir Mchauli Barlotelli aliyemalizia pasi ya Kelvin na kuandika bao hilo la ushindi na mpira kumalizika Academy wakiwa kifua mbele kwa ushindi wa 3-1.

Azam FC waliongia kipindi cha pili Said Morad, Abdulhalim Humud, Omary Mtaki, Himd Mao, KIpre Tchetche, Mwaikimba, Michael Kipre na Ramadhan Chombo 'Redondo'.

Academy iliundwa na Aishi Salum, Dizan Issa, Reina Mgungula/Ismail Adam,Mohamed Hussein, Kelvin Friday, Ally Kaijage/Braison Raphael, Joseph Kimwaga/Jamir Mchaulu, Farid Musa/Abdul Mgaya, Deogratias Names/Ally Aziz na Assad Ally/Ahmed Abbas.

Academy wanatarajia kuondoka nchini Julai 4 kuelekea Burundi kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yatakayoanza Juni 7-21 mwaka huu.