Ratiba ya Ligi  Kuu msimu ujao itatolewa Julai 23 huku mechi za ligi daraja la kwanza (FDL)  zitaanza Septemba 15 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2012/2013 kitamalizika Agosti 10 mwaka huu kulingana na kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya 2012/20.

Uhamisho wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai 30 mwaka huu na kipindi cha kuacha wachezaji (sio wa Ligi Kuu. Wachezaji wa Ligi Kuu wanacheza kwa mikataba) ni kuanzia Juni 15- 30 mwaka huu.

Muda wa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao utaanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

TFF inasisitiza kipindi cha usajili kiheshimiwe na mikoa yote kwa sababu usajili huo huo utatumika katika michuano ya Kombe la FA na hakutakuwa na kipindi kingine cha usajili wa wachezaji kwa klabu zote nchini hadi hapo litakapofunguliwa dirisha dogo.

Imetolewa na Ofisi ya Habari TFF