Wiki mbili kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Kagame, Azam FC wanaendelea kujiwinda kwa mazoezi makali ya ufukweni, gym na uwanjani kwa ajili ya mashindano hayo.

Tovuti ya www.azamfc.co.tz imeshuhudia mazoezi ya timu hiyo chini ya kocha Stewart Hall yakiwa katika hali nzuri wachezaji wakijituma kuhakikisha wanakuwa vizuri.

Programu ya ijumaa iliyopita wachezaji wote (isipokuwa wachezaji 8 waliokuwa Taifa Stars) walianza kwa mazoezi ya kujifua katika gym ya klabu na baadaye mazoezi ya stamina na mwisho wakamalizia kwa kucheza mchezo wa kujipima wao kwa wao.

Mchezo huo ulikua wa kuvutia timu ya kwanza ilikuwa chini ya Abdi Kassim na nyingine ilikuwa inaongozwa na Joseph Owino zote zikatoka sare ya 1-1, magolikipa walikuwa vijana kutoka Azam Academy Aishi Salum na Jackson Wandwi.

Baada ya mazoezi kocha Stewart alisema mazoezi yanaendelea vizuri na program imekuwa na manufaa kwa wachezaji kwa kuwa wamebadilika tofauti na siku waliyoanza mazoezi.

Alisema wachezaji wa Taifa Stars watajiunga na wenzao siku ya Jumatatu kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza michuano hiyo Julai 14 itakayohusisha timu kutoka nchi 10 za Afrika Mashariki na Kati.

Wachezaji waliohudhuria mazoezini Aishi, Wandwi, Said Morad, Michael Kipre, Abdi Kassim, Himid Mao, Ibrahim Shikanda, Luckson Kakolaki, Owino, Jabir Aziz, Abdulhalim Humud, Kipre Tchetche, Abdulghan Gulam, Gaudence Mwaikimba, Ibrahim Mwaipopo, Samir Haji Nuhu, George Odhiambo, Khamis Mcha, Zahor Pazi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

Mchezaji Wazir Salum hakuudhuria mazoezini kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria, program ya mazoezi wiki ijayo, Jumatatu na Alhamis mazoezi ya gym na uwanjani, Jumanne na Ijumaa uwanjani na siku ya Jumatano watafanya mazoezi kwenye fukwe za Coco.