Mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu (VPL) msimu ujao 2012/2013 maarufu kama Ngao ya Jamii ‘community shield’ utachezwa August 25 na kuzikutanisha Azam FC na Simba SC.

Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF), Boniface Wambura alisema baada ya mchezo huo pazia la ligi kuu litafunguliwa Septemba Mosi mwaka huu.

Alisema Ngao ya Jamii ni mchezo unawakutanisha bingwa na mshindi wa pili wa msimu uliopita, hivyo Azam FC ambao ni makamu bingwa wa msimu ulioisha wa 2011/2012 watacheza na Simba waliokuwa mabingwa wa msimu huo kama taratibu za kombe hilo zinavyosema.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza kombe hilo linalochezwa siku chache kabla ya kuanza kwa ligi kuu.

Azam FC inasikia fahari kupata nafasi hii kwa mara ya kwanza na inawaahidi mashabiki wake mchezo makini.