Azam FC imefanikiwa kuingiza wachezaji wanne kati ya tisa wanaowania tuzo mchezaji bora nchini ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) huku Simba ikitoa watatu na Yanga mmoja.

Wachezaji wa Azam FC walioteuliwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja na mfungaji bora John Raphael Bocco na nahodha Aggery Morris wanaowania tuzo za mwanasoka bora pamoja na Juma Kaseja wa Simba.

KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima wa Yanga, atachuana na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC na Mganda Emmanuel Okwi wa Simba kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka wa kigeni nchini ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje wanaoshindana ni Henry Joseph wa Kongsvinger ya Norway na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC na Sophia Mwasikili aliyeko Uturuki.
Kwa upande wa wanawake, Sophia Mwasikili anayecheza Uturuki, anashindana na Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary wote wa Mburahati Queens, Fatuma Mustapha wa Sayari na Eto’o Mlenzi wa JKT.

Wachezaji Chipukizi wanaoshindana ni Shomari Kapombe wa Simba na Salum Abubakar wa Azam FC.