Jezi mpya za Azam FC ambazo zipo katika mchakato wa kutengenezwa zimekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kama Facebook, twitter na Blogs mbalimbali nchini

Mashabiki wengi wa soka wameonekana kuvutiwa na jezi mpya huku wasambazaji wa bidhaa za nguo na baadhi ya maduka wakiomba muongozo wa namna ya kuzipata.

kimsingi Jezi hizi zipo katika mchakato wa kutengenezwa, kwa sasa tunasubiri Sampo kitoka china na baada ya hapo tukilidhika nazo ndipo tutatoa order na inaweza kuchukua hadi miezi miwili kwa jezi kuwa tayari. kwa hiyo mashabiki wasitarajie kwamba zitatoka mapema alisema katibu mkuu wa Azam FC Nassor Idrissa

Azam FC imejijengea heshma kwa kwa kuwa inatoa toleo jipya la jezi kila msimu huu ukiwa ni msimu wake wa tatu ambapo msimu uliopiza Jezi hizo zilidhaminiwa na Azam Cola na msimu huu itakuwa Azam Energy Drink

 

http://bongostaz.blogspot.com/2012/05/azam-fc-waja-na-uzi-upya-mkali-wa.html

 

http://kandanda.galacha.com/5206/featured/simba-yanga-mpo-azam-na-uzi-wao-mpya

 

http://www.facebook.com/azamfc

 

http://www.facebook.com/?ref=tn_tnmn#!/groups/kandanda/