Luckson Jonathan Kakolaki amekuwa mchezaji wa mwisho kufunga dirisha la usajili kwa Azam FC msimu wa 2012/13. Kakolaki, beki kisiki ambaye amekuwa na Azam FC toka madaraja ya chini hadi ligi kuu mwishoni mwa wiki iliyopita alishinda tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu wa Azam FC alimwaga wino wa kuichezea Azam FC mwanzoni mwa wiki na kumaliza uvumi ulioanza kutanda kuwa kuna timu moja kubwa ilikuwa ikimnyatia.

Pia kukamilishwa kwa usajili kunavunja tetesi zilizozagaa mitaani kuwa kuna wachezaji wa Azam FC watakaotimkia timu flani au wachezaji wa timu flani kutakiwa kujiunga na Azam FC.

Tofauti na msimu uliopita ambapo Azam FC ilisajili nyota wapya 11 na baadaye kuongeza wengine wanne hapo Disemba na kufikisha jumla ya wachezaji 15 wapya, Msimu ujao Azam FC imeongeza wachezaji wawili tuu ambao ni George Blackberry Odhiambo toka Randers FC ya Denmark na Deo Munishi Dida toka Mtibwa Sukari ya Manungu.

Kwa maana hiyo Azam FC imesajili wachezaji 27 na haijaacha mchezaji hata mmoja ingawa mwalimu Stewart Hall ameacha maagizo ya kupelekwa kwa mkopo wachezaji wanne, ambapo wa kiungo katikati ni wawili, kiungo pembeni mmoja na golikipa mmoja ili kuwapa nafasi ya kucheza kutokana na mlundikano wa wachezaji kwenye nafasi hizo.

Azam FC ambayo itawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa hapo mwakani inajivunia kikosi ilichonacho na usajili huu ulikuwa na lengo la kuziba mapengo yaliyoachwa wazi ambapo Blackberry anachukua nafasi ya Mghana Wahab Yahaya na Dida anachukua nafasi ya golikipa Mserbia Obren Cuckovic.

Azam FC inajivunia kurudi na kupona 100% Mlinzi Joseph Owino Gere ambaye atanza kuonekana uwanjani kuanzia msimu ujao. Pia Azam FC inajivunia nyota wake wa Under 20 ambao imewapandisha juu ambao ni Aishi Salum, Juckson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga.

Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi

Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu

Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris

Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo

Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry" Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"