Kikosi cha vijana cha Azam Academy  jana kilishinda mechi yake ya tatu mfululizo 1-0 dhidi ya mabingwa wa ligi daraja la kwanza BZL mchezaji Assad Muda Maliga akifunga katika kipindi cha pili.

Kikosi hicho cha vijana kilichopo kisiwana Zanzibar kwa ziara ya siku nne leo kitacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar Under-20 huu ukiwa mchezo wake wa mwisho wa kirafiki.

Wakati huohuo kikosi cha Azam FC leo kitashuka katika dimba la uwanja wa Jamhuri kukwaana na Polisi Dodoma katika muendelezo wa ligi kuu Vodacom ikiwa na raudi ya 23.

Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 ipo katika harakati za kuhakikisha inashika moja kati ya nafasi mbili za juu ili iweze kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michezo ya Afrika.

Kulingana na mazoezi ya jana asubuhi, kikosi kitakachoanza leo ni Mwadini Ally, Ibrahim Shikanda, Waziri Salum, Aggrey Morris, Said Moradi, Jabir Aziz, Kipre Bolou, Salum Abubakar, John Bocco, Kipre Tchetche na Mrisho Ngasa