Azam Academy wameishushia kipigo cha 2-1 timu ya Simba B katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo imevuta hisia za mashabiki wa timu hizo na kukumbushia mchezo wa fainali ya kombe la Uhai kwa vijana wa timu za ligi kuu ambapo Simba walishinda kwa peneti ya 5-6.

Katika mchezo huo timu zote zilicheza kwa ushindani na kukumbushia fainali hizo, Azam walipata goli la kwanza mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Ally Mnasi na kudumu hadi mapumziko.

Azam walidhirisha kuwa wao wapo vizuri kwa kucheza kandanda safi huku wakijifua maalum kutaka kurudisha kombe hilo mwaka huu.

Kelvin Friday aliifungia Azam goli la pili dk 62 kwa mkwaju wa penati baada ya mabeki wa Simba kuunawa mpira katika eneo la penati.

Baada ya kufunga goli hilo Kelvin alitolewa kwa  kadi nyekundu, dakika moja baadae dk 79 Ramadhan aliifungia Simba goli la kufutia machozi.

Azam Academy wataondoka siku ya Jumanne kuelekea visiwani Zanzibar kwa kambi ya siku nne.

Wakiwa visiwani humo watacheza mechi mbili za kirafiki na kurejea jijini April 14.