Azam FC Academy itashuka dimbani kukwaana na Simba B kesho jumamosi tarehe 07/04/2012 saa kumi jioni mchezo ukichezwa kwenye uwanja wa Karume jijini zilipo ofisi za TFF.

Huu utakuwa mchezo muhimu kwa vikosi hivi vya vijana ambavyo vinasifika kucheza soka la kuvutia linalovuta hisia za mashabiki wengi.

Simba B ambao ni mabingwa wa Uhai Cup wamekuwa na upinzani mkali na Azam FC Academy hii ni kutokana na ukweli kwamba Azam FC Academy ndiyo timu pekee ambayo imekuwa na mafanikio makubwa zaidi kwenye mashindano ya vijana ikiwa na wachezaji wengi zaidi kwenye vikosi vya timu za taifa za Under17 na Under20 huku kikiwa kinashikiria rekodi ya kutwaa Uhai Cup mara mbili na mara moja mwaka jana kufika fainali ambapo ilifungwa na Simba kwa penati 5-4