Kwa mara ya kwanza leo tangia nianze kutazama mechi za Azam FC nimeshuhudia timu ikicheza kwa ari kubwa na ikipania kupata ushindi na juhudi zao zimepelekea timu kupata ushindi wa 4-1.

Ushindi wa 4-1 dhidi ya JKT Ruvu umeipeleka Azam FC nafasi ya pili na kuiacha Yanga ambayo jana ilimchezesha Nadir Haroub Canavaro kimakosa kwenye nafasi ya tatu.

Mchezo huo umechezwa kwenye uwanja wa Azam Chamazi, na kushudia John Bocco akiendelea kuongeza idadi ya magoli ya kufunga na kufikisha magoli 16 akiongoza wafungaji ligi kuu.

Bocco leo amefikia rekodi ya klabu iliyowekwa na Mrisho Ngasa na sasa anatafuta nafasi ya kuvunja rekodi ya ligi kuu ambayo inashikiliwa na Boniface Ambani aliyewahi kufunga magoli 18.

Katika mchezo huo JKT Ruvu walikua wa kwanza kupata goli katika dakika ya 7 kupitia kwa Hussein Bunu, goli liliamsha kasi kwa Azam FC huku JKT wakidhani wamemaliza mchezo.

Mrisho Ngasa alifungua kalamu ya magoli dk 25 kwa kuipatia Azam FC goli la kwanza akimalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Bocco.

Goli hilo la kusawazisha liliamsha kasi ya mchezo huo, dk 40 Bocco aliandika bao la pili kwa Azam FC akitumia vema mpra uliopigwa na Ngasa na kumgonga beki JKT ukatua miguuni kwake na kuandika goli hilo lililopeleka mapumziko Azam wakiongoza 2-1.

Kipindi cha kwanza mwamuzi Oden Mbaga alimtoa mchezaji wa JKT, Amos Mgisa kwa kumuonyesha kadi nyekundu dk 31 baada kumtendea madhambi Kipre Bolou.

Kipindi cha pili Azam FC walianza kwa kasi dk 49 Kipre Tchetche alifunga bao la tatu kwa kichwa akimalizia mpra wa kona uliopigwa na Ngasa.

Ngasa alihitimisha idadi ya magoli kwa kupachika goli la nne katika dk 69 akimalizia mpra wa Tchetche na kupiga shuti lililompita kipa wa JKT, Hamis Satifu na kumaliza Azam FC wakitoka na ushindi wa 4-1.

Azam wamefikisha pointi 47 na kurudi nafasi ya pili ikiwa chini ya Simba wenye pointi 50, huku Yanga ikiwa nafas ya tatu kwa kuwa na pointi 46.

Azam, Mwadini, Waziri Salum, Agrey Moris, Erasto Nyoni, Said Morad, Sure Boy Salum, Michael Kipre/ Khamis Mcha dk 66, kipre/Mwaikimba dk 72, Abdi Kasim/Humud dk 25, Ngasa na Bocco.