Raundi ya 22 ya ligi kuu ya Vodacom inaingia leo jioni kwa klabu ya Azam FC  pale itakapokwaana na JKT Ruvu lakini klabu ya Simba imeshaingia jana kwa ushindi wa 2-0 dhdi ya African Lyon FC.

Kwa klabu nyingine yenye matumaini ya kunyakua taji la ligi kuu Yanga, yenyewe jana ilicheza mchezo wake wa 21 dhidi ya Coastal Union na kushinda 1-0 lakini kwa taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari nchini ni kwamba mchezo huo uliingia dosari kwa Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub Canavaro ambaye alikuwa na kadi nyekundu aliyoipata kutokana na vurugu dhidi ya mwamuzi na alistahili kukosa mchezo wa jana.

Azam FC leo itaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kuhakikisha inashinda ili kuendeleza na kuweka hai matumaini yake ya kuhakikisha inanyakua moja ya nafasi mbili za juu.

Baada ya mchezo wa leo Azam FC itabakiwa na michezo minne dhidi ya Polisi ya Dodoma kule Dodoma, kasha kurejea Dar es Salaam kumalizia na Mtibwa Sugar, Toto Africa na kagera Sugar.