Yanga leo imeifunga Villa Squad 1-0 na kukwea hadi nafasi ya pili ikiishusha Azam FC nafasi moja lakini Azam FC itakuwa uwanjani kesho kukwaana na Ruvu Shooting Stars. Katika mechi nyingine ya VPL Coastal Union imeifunga JKT Oljoro na kukwea hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu.

Katika mchezo wa Kesho Azam FC itamkosa beki wake mahiri Said Moradi aliye na kadi tatu za njano na nafasi yake inatazamiwa kuzibwa na ama Luckson Kakolaki au Erasto Nyoni kutegemea na maamuzi ya kocha. Ukiondoa Moradi wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wanasubiri mchezo wa kesho utakaofanyika Azam Stadium-Chamazi

Katika mchezo wa kesho viingilio vitakuwa Tsh. 10,000 kwa jukwaa kuu na Tsh. 1,000 kwa mzunguko

Siku hiyi hiyo ya kesho Simba watakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri kukwaana na Mtibwa Sugar