Kikosi cha Azam FC kinachoshika nafasi ya tatu kwenye mbio za kuusaka ubingwa wa ligi kuu leo kimeingia kambini kijiandaa na mchezo kati yake na timu iliyo katika kiwango cha juu ya Coastal Union ya Tanga.

Kambi ya safari hii ni ndefu zaidi kufanywa na Azam FC kwani baada ya mchezo wa jumatano dhidi ya Coastal Union ya Tannga, kambi hii itaendelea hadi baada ya mchezo dhidi ya Yanga utakaofanyika jumamosi ijayo.

Wachezaji wote wa Azam FC wameingia kambini isipokuwa wachezaji wawili ambao ni Ramadhan Chombo Redondo ambaye hajulikani aliko na Joseph Owino Gere ambaye ni majeruhi.

Kikosi cha Azam FC kinaweza kumkosa Khamis Mcha Khamis Viali ambaye pia ana maumivu ya kifundo na anaendelea na matibabu. Ukiondoa wachezaji hao wachezaji wengine wote wapo katika hali nzuri.