Timu ya Azam FC imepoteza mchezo wake wa ligi kuu baada ya kufungwa 2-0 na Simba SC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam.

Matokeo hayo yameibakisha Azam katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32.

Katika mchezo huo Azam walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata vipindi vyote viwili na kuwapa nafasi Simba.

Magoli yote ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi dk 29 na 67 kutokana na uzembe wa mabeki wa Azam.

Azam itashuka uwanjani siku ya Jumatano wiki ijayo kucheza na Villa Squad katika uwanja wa Azam, Chamazi