Stewart Hall tangia atue nchini amekuwa na rekodi nzuri sana dhidi ya Simba SC ambayo amecheza nayo mara tatu na kushinda mara mbili huku akitoka sare mara moja. Leo jioni kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 04:00 kikosi cha Azam FC kitashuka dimbani kuivaa Simba SC

Endapo Azam FC itashinda mchezo wa leo basi ni dhahili Azam FC itaongoza ligi hata kama itakuwa ni kwa masaa ikisubiri mtanange kati ya Yanga na Ruvu Shooting kesho.

Kambi ya Azam FC ipo katika hali nzuri sana na vijana wameahidi ushindi, Club ya Azam FC inaomba mashabiki kuwa watulivu na wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huu wa leo ambao utatoa muelekeo wa Ubingwa wa Tanzania na kuchangamsha ligi

Mungu Ibariki Azam FC, Mungu wabariki wachezaji na viongozi wa Azam FC

Webmaster