Goli pekee la mshambuliaji mahiri wa Azam FC, John Bocco limeipatia Azam FC pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu baada ya kuifunga Moro United 1-0, mchezo uliochezwa leo uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam FC walipata ushindi huo wa pili mfululizo katika mzunguko huu wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom, VPL msimu wa 2011/2012 na kufikisha jumla ya pointi 29 katika msimamo wa ligi hiyo.

Bocco amefunga goli hilo katika dakika ya 11 ya mchezo akitumia uzembe wa mabeki wa Moro na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Moro, Jackson Chove.

 Kufuatia goli hilo, Bocco anaongoza wafungaji katika ligi kuu kwa kufikisha magoli 10 akiwa mbele ya Keneth Asamoah wa Yanga mwenye magoli 9.

Azam walianza kutafuta goli mapema ndani ya dakika tano za kwanza walifanya mashambulizi matatu ambayo hayakuzaa matunda.

Baada ya goli hilo Moro United walifanya mashambulizi  wakitaka kusawazisha dakika ya 21 Kelvin Charles alipiga mpira wa adhabu ukaokolewa na kipa Mwadini wa Azam na kipindi cha pili Simon Msuva anayeichezea Moro United kwa mkopo akitokea Azam FC, alifanya mashambulizi mawili dakika ya 60 na 86 lakini hakuweza kubadilisha matokeo hayo.

Azam walitengeneza nafasi nyingi walikosa kumalizia, Kipre Tchetche akiwa na kipa Chove alishindwa kufunga katika dakika ya 25 na Mrisho Ngassa alishindwa kufunga dakika ya 63.

Mabadiliko katika mchezo huo Azam waliwarejesha benchi dk 60,  dk 75 Abdi Kassim ‘Babi’ na na Kipre Tchetche nafasi zao zikichukuliwa na Ibrahim Mwaipopo na Zahoro Pazi na baadaye  dk 77 John Bocco akampisha Gaudence Mwaikimba.

Kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema matokeo ya mchezo huo yanatoa nafasi ya kujiweka vyema katika kumalizia mzunguko huu, japokuwa timu yake haikufanya vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Akizungumzia kukosekana ka Michael Kipre pacha wa Tchetche alisema bado hati yake ya kucheza ligi ya Tanzania bara bado haijawasili kutoka nchini Ivory Coast. Stewart alisema pengo la Kipre ni kubwa sana

Mbali na mchezaji huyo beki Erasto Nyoni hakuweza  kucheza kutokana na kufiwa na mama yake mzazi hali iliyopelekea wachezaji wa Azam FC kuvaa vitambaa vyeusi wakati wa mechi.

Kikosi Azam FC, Mwadini Ally, Aggre Moris, brahim Shikanda, Wazir Salum, Said Morad, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Abdulhalim Humud, Abdi Kassim/Zahor Pazi, Mrisho Ngassa, Kipre Tchetche/Ibrahim Mwaipopo na John Bocco/Gaudence Mwaikimba.

Moro Jackson Chove, Tumba Swed, Fred Mbuna, Salum Kanoni, Meshack Abel, Gideon Sepo, Godfrey Wambura, Hilali Bingwa, Kelvin Charle/Simon Msuva, Benedict Ngassa na Andrew Kas