Kikosi cha Azam FC jana kiliingia kambini ikiwa ni maalum kwa kuanza mechi za kumalizia mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom VPL.

Azam FC itaanza mchezo wake wa kwanza katika mzunguko huu dhidi ya African Lyon utakao chezwa siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Azam, Chamazi.

Kikosi hicho kimefanya mazoezi ya viungo wikiendi iliyopita kwenye ufukwe wa Coco beach, kimeendelea na mazoezi ya kiufundi kwenye uwanja wa klabu.

Mazoezi hayo yamehudhuriwa na wachezaji wote 23 waliokuwa Zanzibar kwenye mapinduzi Cup, lakini Abdulghani Gulam aliyepata majuruhi yeye alikuwepo kambini lakini hakufanya mazoezi, wachezaji wote wameingia kambini katika hostel za timu zilizopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Azam FC kina wachezaji 25, kwa maana hiyo wachezaji ambao hawapo kambini ni Joseph Owino ambaye anaendelea na mazoezi maalum baada ya kurejea kutoka kwenye majeruhi na Ramadhani Chombo Redondo ambaye hapo awali alisimamishwa kwa mwezi mmoja kutokana na utovu wa nidhamu na adhabu yake kumalizika Januari 16 lakini hadi sasa hajaripoti kambini.

Katika mazoezi ya jana asubuhi wachezaji walitumia muda mwingi kufanya mazoezi ya kupiga mashuti ya mbali na viungo, kupiga mipira ya kichwa na kupokea mipira kwa washambuliaji na wafungaji.

Jioni kwa muda wa saa moja wachezaji walifanya mazeozi ya kupiga kona na mipira ya iliyokufa 'free kicks' maalum kwa kujiandaa na michezo ijayo.

Kocha wa kikosi hicho Stewart Hall amesema mazoezi hayo ya aina tatu tofauti yatawasaidia wachezaji kuhimili michezo yote katika mzunguko huu.

Wachezaji waliongia kambini ni magolikipa Mwadini Ally na Aishi Salum, walinzi ni Aggrey Moris, Erasto Nyoni, Said Morad, Luckson Kakolaki, Wazir Salum, Samir Haji Nuhu na Ibrahim Shikanda.

Viungo Abdulhalim Humud, Himid Mao, Michael Kipre, Abdi Kassim 'Babi', Salum Aboubakar 'Sure Boy', Jabir Aziz na Ibrahim Mwaipopo, washambuliaji ni Mrisho Ngassa, Zahor Pazi, Gaudence Mwikimba, Tchetche Kipre, John Bocco na Khamis Mcha