Azam FC hapo jana jioni ilidhihirisha ubora wake baada ya kuendeleza ushindi kwa kuifunga Villa Squad 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa saba kwa Azam FC kucheza bila kufungwa, michezo hiyo ya kirafiki pamoja na michezo ya kombe la Mapinduzi, timu hiyo imetoka sare mchezo mmoja.

Katika mchezo huo Azam FC walichezesha vikosi viwili katika timu yao, kikosi cha kwanza kilikuwa chini ya nahodha Aggrey Moris kilianza kupata goli katika dakika ya 8 lililofungwa na mshambuliaji bora wa Mapinduzi Cup, John Bocco.

Kikosi hicho kilichocheza kipindi cha kwanza kilikuwa na golikipa Aishi Salum, Morris, Said Morad, Salum Wazir, Abdulhalim Humud/Himid Mao, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Michael Kipre, Erasto Nyoni, Mrisho Ngassa, Kipre Tchetche na Bocco, kikosi kilimaliza kipindi cha kwanza kwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili Azam FC waliingiza na sura mpya wakiwa chini ya nahodha Ibrahim Shikanda waliongeza maumivu kwa timu hiyo katika dakika ya 56, Gaudence Mwaikimba aliipatia Azam goli la pili kwa shuti lililomshinda kipa Daudi Mwasongwa wa Villa Squad ambaye yupo kwa mkopo akitoke Azam FC.

Mwaikimba akicheza vizuri pamoja na Abdi Kassim na Khamis Mcha aliipatia Azam goli la tatu kwa shuti lililotinga moja kwa moja wavuni.

Kikosi hicho cha pili katika mchezo huo kilionekana kusumbua muda wote wa dakika kipindi cha pili kililiundwa na golikipa namba moja wa Azam, Mwadini Ally, Shikanda, Luckson Kakolaki, Abdulghan Gulam, Ibrahim Mwaipopo, Samir Haji Nuhu, Jabir Aziz, Abdi Kassim, Khamis Mcha, Mwaikimba na Zahor Pazi.

Villa walipata goli dakika ya 85 lililofungwa na Ally Manzi, wachezaji wa Villa, Cosmas Lewis, Haruna Shamte, Malika Ndeule, Nsa Job na Luseke Kiggi walionesha uimara wa timu yao.

Mchezo huo wa kirafiki imechezwa siku nne kabla ya kuanza mzunguko wa kumalizia ligi kuu ya Tanzania bara utakaoanza Januari 21.