Baada ya kuitoa Yanga kocha wa Azam FC amesema sasa ni zamu ya kuitoa Simba katika mchezo wa nusu fainali itakayochezwa leo usiku kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Simba imeingia hatua hiyo na kukutana na Azam FC kingekewa huku ikiacha simulizi lukuki kutokana na kiwango chao, kocha Stewart Hall wa Azam amesema walishajiandaa muda mrefu kukutana na moja kati ya timu hizo.

“Imekuwa kama hali ya kushangaza kwetu, kukutana na Simba na Yanga katika michuano hii, mwanzo tulijiandaa kukutana na moja ya timu hizi kabla ya kuingia fainali, hivo tumekutana nazo zote” alisema Stewart.

Aliongeza kuwa ili kufika fainali wanahitaji kuitoa Simba katika mchezo wa kesho kitu ambacho wameshajiandaa nacho na wapo kamili kwa ajili ya kucheza mchezo huo.

“Hii ni mechi nyingine ngumu kwetu kukutana nayo, tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunavuka hatua hiyo na kuingia fainali najua Simba watajiandaa lakini sie tuejiandaa zaidi” alisisitiza Stewart.

Alisema wachezaji wana ari ya ushindi na kila mtu anaonesha nia ya kutaka kushinda katika mchezo huo utakaotupatia nafasi ya kuingia fainali.

Kocha amesema mchezaji Mrisho Ngassa aliyekosa mechi iliyopita amesharejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupatiwa matibabu. kikosi kamili kitapanga baadaye leo.

Azam ikishinda mchezo huo itacheza fainali na mshindi wa mechi kati ya Mafunzo na Jamhuri itakayochezwa siku ya Jumanne.