Nahodha Agrey Morris amewatoa shaka mashabiki wa Azam FC kwa kuhakikisha ushindi katika mchezo dhidi ya Yanga uliopangwa kuchezwa kesho usiku kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Azam kesho itashuka uwanjani kumalizia mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa.

Aggrey alisema wachezaji kwa pamoja wapo sawa kwa mechi hiyo hawaogopi wala kuhofia kitu chochote zaidi kuhakikisha kupata ushindi katika mchezo huo muhimu utakaowapeleka hatua ya nusu fainali.

“Sisi tumejiandaa tangu muda mrefu kwa ajili ya timu yoyote, lengo letu ni kushinda na kufikia malengo yetu, tupo tayari kucheza na Yanga na timu nyingine yoyote” alisisitiza Aggrey.

Nahodha huyo aliongeza kuwa kujituma kwa wachezaji wote kutakuwa sehemu kubwa ya mafanikio yao katika kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Azam FC wanatakiwa kupata sare aina yoyote kuvuka kucheza hatua hiyo huku wapinzani wao Yanga wakiwana  kibarua kigumu cha kulazimika kuifunga Azam FC ili kuvuka.

Msimu uliopita Azam FC ilitolewa na Yanga katika mazingira kama ye Kesho baada ya kukubali kipigo cha 2-1

Azam imeendelea na mazoezi ya ufukweni wanakofanya kila siku,

Timu hizo zinakutana kwa mara ya tatu katika michuano mitatu tofauti Azam wakiwa wameshinda michezo yote miwili.