Kiungo Ramadhan Chombo Redondo ameamua kubaki Azam FC lakini kikosi cha Azam FC kimenogeshwa kwa kuongezewa Abdi Kassim 'Babi' ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Azam FC kwa miezi 18 na kuungana na Gaudensi Mwaikimba, Joseph Owino Gere na Bolou Michael Wilfred Kipre ambaye ni pacha na Kipre Tchetche

Babi ameingia mkataba huo baada ya kuwasiliana na kocha wake Stewart Hall na kumueleza kuwa yupo huru na angependa kujiunga na Azam FC.

Babi amejiunga na Azam FC kama mchezaji huru baada ya kuachwa na timu ya DT Long An ya Vietnam iliyoshuka daraja msimu uliopita, kabla ya kujiunga klabu hiyo Badi alikuwa mchezaji wa Yanga ya Dar es Salaam.

Kipre Bolou na Babi wataungana na Gaudence Mwaikimba nyota aliyesajiliwa ili kuongeza idadi ya magoli Azam FC na Joseph Owino mchezaji ambaye Azam FC ilimsajili mwezi May mwaka huu kasha kumpeleka India kwa matibabu ya goti na sasa amerejea na anaanza matibabu ya viungo chini ya daktari wa Azam FC.

Mbali na wachezaji hao klabu imewapandisha wachezaji wanne kutoka Azam Academy. Kufanya mazoezi na kikosi cha wakubwa, wachezaji hao ni Aishi Salum ambaye ni golikipa, Kelvin Friday ambaye ni mshambuliaji, Dizana Issa ambaye ni mlinzi na Mohamed Hussein ambaye ni beki wa kushoto.

Aidha klabu imewapeleka kwa mkopo wachezaji nane, watano kati yao wakitoka kikosi cha vijana cha Azam FC,(waliotoka timu ya wakubwa majina yao wino umekolezwa) walioenda Moro United ni Jamal Mnyate na Simon Msuva, watakaocheza Villa Squad ni Ismail Gambo, Malika Ndeule, Fred Cosmas, Daudi Mwasonwe na Ibrahim Rajab, wakati mchezaji Omary Mtaki anakwenda JKT Oljoro.

Aidha wachezaji Wahab Yahaya na Nafiu Awudu ambao walisajiliwa kwa mkopo Azam FC walisharuhusiwa kurudi nyumbani.