Juhudi vipaji na umakini wa wachezaj wa Azam Academy, umeipeleka timu hiyo katika fainali za Kombe la vijana 'Uhai Cup' baada ya kuifunga Serengeti Boys (U17) 3-0.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Karume, Azam Academy watakutana Simba B katika mechi ya fainali kuwania bingwa wa michuano hiyo. mchezo utakaochezwa kwenye uwanja huo huo.

Azam wakiwatumia vyema wachezaji wake, mshambuliaji anayekuja kwa kasi Simon Happygod Msuva alifunga magoli yote matatu (hat trick) na kuweka rekodi ya kwanza kufunga idadi hiyo ya magoli katika mechi moja.

Msuva alianza kuisumbua ngome ya Serengeti iliyokuwa chini ya kipa Juma Hamad kwa kufunga goli la kwanza dk 39 akiunga mpira mfupi wa mchezaji Kelvin Idd.

Dk 42 Msuva aliandka goli la pili kwa kichwa akitumia vyema uzembe wa mabeki wa Serengeti Boys, matokeo hayo Azam walitoka mapumziko wakiwa kifua mbele kwa 2-0.

Kalamu ya magoli ilihimishwa dak 47 kwa Msuva kufunga goli jingine la kichwa akipokea mpira wa Ally Kaijage.

Katika mchezo huo Azam walionesha kiwango cha juu wakiongozwa na kiungo Ibrahim Juma 'Jeba' aliyetokea safarini nchini Misri akiwa na timu ya taifa ya Zanzibar.

Mwamuzi wa mchezo Liston Hiyari alimpa kadi nyekundu mchezaji wa Azam Eliminus Ryeyna kwa kosa la kutendea madhambi mchezaji Farid Musa wa Serengeti Boys.

Pia Kocha Jamhuri Kihwelu naye alitolewa uwanjani na mwamuzi kutokana na kutoa lugha chafu.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, Simba waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Toto African, hivyo Toto watakutana Serengeti Boys katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu, timu hizo zinakutana kwa mara ya pili katika michuano ya mwaka huu baada ya kukutana kweye hatua ya makundi na kutoka sare.

Hii ni fainali ya tatu kwa Azam Academy katika mashindani ya nne ya Uhai Cup iklitwaa kombe hili mara mbili huko nyuma

Azam walitinga fainali Aishi Mfulila, Mgaya Jafari, Ally Kaijage, Ibrahim Juma 'Jeba'/ Mussa Kanyaga, Asad Ally, Dizana Yarouk, Braison Nkulula, Kelvin Idd, Mohamed Hussein, Msuva na Eliminus Ryeyna]