Timu ya Azam Academy leo imemvua ubingwa Ruvu Shooting baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa makundi na kuipeleka Azam kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya vijana chini ya miaka 20 kwa vilabu vya ligi kuu 'Uhai Cup 2011'.

Mchezo huo uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume, Azam Academy walikuwa wakihitaji pointi moja kuingia hatua hiyo wakati Ruvu Shooting wakitakiwa ushindi aina yoyote, Shooting walitwaa kombe hilo msimu uliopita wameshindwa kulitetea vyema kombe lao na kuliacha huku wakiyaaga mashindano hayo hatua za makundi.

Katika mchezo huo Azam walitumia vipindi vyote kuimarisha ulinzi na kutoruhusu goli lolote hivyo hadi vipindi vyote kumalizika timu zilitoka suluhu iliyokuwa na manufaa kwa Azam.

Azam wameingia hatua hiyo pamoja na timu ya JKT Oljoro ambayo inaongoza kundi hilo 'A' kwa kuwa na pointi 8 ikifuatiwa na Azam FC na Kagera Sugar zenye pointi tano tofauti ya magoli ya kufunga.

Ruvu Shooting imeaga mashindano hayo pamoja na Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Polisi Dodoma na Coastal Union, wakati timu zingine zilizoingia robo fainali inayorajiwa kuanza Jumatatu Nov 21 ni Moro United na Serengeti Boys (U17).

Azam watacheza mechi ya robo fainali na mshindi wa pili wa kundi B kwenye uwanja wa Azam Chamazi.

Azam: Aishi Mfula, Mange Gugah, Brison Mkulula, Samwel Mkomola/