Timu ya Azam Academy hapo jana ilianza vyema michuano ya vijana chini ya miaka 20, kwa vilabu vya ligi kuu 'Uhai Cup 2011' kwa kuifunga Kagera Sugar 2-1 katika mchezo uliochezwa asubuhi kwenye uwanja wa Azam Chamazi.

Azam Academy walianza mapema kulisakama lango la Kagera na kufunga goli la kwanza dakika ya kwanza lililowekwa wavuni na Mange Gugah.

Goli hilo la kwanza kufungwa kwenye mashindano hayo, liliamsha nguvu kwa Azam ambao walitawala mchezo na kutoka mapumziko wakiwa mbele 1-0.

Azam walipata goli la pili dk 67 lililofungwa na Simon Happygod kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa Kagera, Adam Osea.

Goli la Kagera lilipatikana dk 78 kupitia kwa Faudhu Abdul. Matokeo hayo yameipa point tatu Azam Academy ambayo itakua sawa na Jkt Oljoro iliyoifunga Ruvu Shooting 2-1, zote za kundi A.

Azam itacheza mchezo wake wa pili, Jumatano dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Azam.

Azam Academy, Aishi Salum, Mgaya Abdul, Mohamed Hussein, Samwel Nkomola, Dizana Issa, Braison Nkulula, Ellyminus Reyna, Assad Musa, Mange Gugah/mwinyi Jamal, kelvin Friday/Gadson Naftari na Simon Happyg