Timu ya Azam FC imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kwa kutoka sare ya 1-1 na Toto African katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Kwa matokeo hayo ya mchezo huo wa mwisho kwa mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2011/2012, Azam FC imemaliza mzunguko huo kwa kufikisha pointi 23. Ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Simba yenye pointi 28 na Yanga yenye pointi 27

Katika mchezo huo, Toto Africa walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya tisa lililofungwa na Philemon Mwendasile aliyepiga shuti likamteleza kipa Mwadin Ally na kuingia wavuni.

John Bocco aliongeza goli lake la nane kwenye ligi kuu kwa kuifungia Azam goli la kusawazisha dk 45 kwa mkwaju wa penati iliyopatikana baada mabeki wa Toto kumwangusha Mrisho Ngassa kwenye eneo la penati.

Bocco amefikisha idadi hiyo ya magoli sawa na mchezaji Keneth Asamoah wa Yanga, Bocco amekuwa mchezaji mwenye uwezo unaoongezeka kadri muda unavyokwenda.

Katika mchezo huo mchezaji Samir Haji Nuhu amerejea katika kiwango chake kwa kucheza vipindi vyote viwili, Haji alikuwa nje ya uwanja kwa miezi sita kutokana na kufanyiwa upasuaji wa goti nchini India mapema mwaka huu.

Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Ibrahim Mwaipopo na Zahor Pazi wakaingia Khamis Mcha Vuali na Salum Aboubakar, mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Azam FC na kubadili mchezo lakina yahakuleta matokeo.

Baada ya mchezo timu ya Azam FC imesafiri kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ndege ya usiku.

Kikosi cha Azam FC kilichomaliza mzunguko wa kwanza , Mwadini Ally, Haji, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Said Morad, Ibrahim Mwaipopo/Khamis Mcha, Rmadhan Chombo Redondo, Mrisho Ngassa, Zahor Pazi/Salum Aboubakar, Mrisho Ngassa na John Bocco