Timu ya Azam FC iliwasili salama mkoani Kagera jana asubuhi tayari kwa maandalizi ya mchezo wake wa 12 wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani hapa.

Hapo jana Azam FC ilifanya mazoezi kwenye uwanja wa shule ya Seminari Bukoba kabla ya leo asubuhi kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba

Azam FC itacheza mchezo huo kabla ya kucheza mchezo wa mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza siku ya Jumatano dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza.

Kikosi kamili cha Azam FC kiliwasili mjini mwanza alfajiri ya alhamisi kwa ndege ya shirika la ndege la Precissions kutokea mkoa Dar es Salaam kisha ikapumzika kwa masaa kwenye hoteli ya Sparrow kabla ya kupanda meli ya MV Victoria kuelekea Bukoba ambapo iliwasili salama na kuweka kambi kwenye hoteli ya Smart jijini hapa.

Azam FC ilipoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar, beki wa Azam, Erasto Nyoni amesema timu imejiandaa vizuri wamerekebisha makosa yaliyotokea kwenye mchezo huo na anadhani watafanya vizuri.

Akizungumzia hali ya hewa ya Kagera, Nyoni amesema Kagera kuna hali ya ubaridi tofauti na Dar es Salaam lakini hawatarithika na hali hiyo kwa kuwa wamejiandaa kikamilifu na wapo tayari kucheza katika hali yoyote ya hewa.

Baada ya kumalizika mchezo huo timu ya Azam FC itaelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mwisho dhidi ya Toto African.

Wachezaji waliopo Kagera tayari kwa mchezo huo, Mwadini Ally, Obren Cuckovic, Erasto Noni, Ibrahim Shikanda, Said Morad, Aggrey Morris, Ibrahim Mwaipopo, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Jabir Aziz, John Bocco, Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo Redondo’, Luckson Kakolaki, Zahor Pazi, Abdulhalim Humud, Tchetche Kipre, Samih Ally Nuhu, Khamis Mcha, Abdulghani Ghulam Abdallah na Himid Mao.