Klabu ya Azam FC kwa mara ya kwanza katika historia yake imafanikiwa kuvunja mwiko wa kuishia pointi ishirini (20) kwenye msimamo wa ligi kuu VPL raundi ya kwanza

Licha ya safari hii ligi kuwa na timu 14, ambazo ni nyingi ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita, lakini ukweli ni kwamba Azam FC imecheza michezo 10 tuu hadi hivi sasa ikiwa imejikusanyia pointi 21, lakini msimu uliopita ilimaliza raundi ya kwanza ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza michezo 11.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo TFF, Yanga wao msimu uliopita walimaliza wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 11 lakini msimu huu wana pointi 21 baada ya kucheza michezo 11, wakiwa na pointi nne (4) pungufu ya zile walizopata msimu uliopita

Simba wao walimaliza raundi ya kwanza msimu uliopita wakiwa na pointi 27 baada ya kucheza michezo 11 na msimu huu tayari wameshafikisha pointi 27 baada ya kucheza michezo hiyohiyo hivyo basi kuirudia rekodi yao.

Licha ya kufikisha pointi 21, huku wakiwa na michezo mitatu mkononi, Azam FC pia imeweka rekodi nyingine ikiwa haijapoteza mchezo kwa vilabu vya Simba na Yanga katika raundi ya kwanza. Kwa kawaida Azam FC ilikuwa na desturi na kufungwa angalau mchezo mmoja na kujitutumua na kutoka angalau sare mchezo mwingine huku ikipata angalau ushindi kwenye mechi moja msimu mzima toka kwa wakongwe hawa wa ligi kuu.

Rekodi nyingine iliyovunjwa na Azam FC ni ya nyavu zake kutikiswa mara chache zaidi huku kambi yake ikionekana kuwa nautulivu na upendo wa hali ya juu baina ya wachezaji

Kuna haja ya kusubiri hadi mwisho wa raundi ya kwanza ili kujiua Azam FC itavuna pointi ngapi raundi hii na kwa namna gani pointi hizi zitaisaidia Azam FC kwenye msimamo wa ligi Apri mwakani

http://www.azamfc.co.tz/league_standings