Tovuti ya Azam FC yafikisha hits milioni tatu

Inawezekana tovuti ya Azam FC ikawa ndiyo tovuti inayotembelewa zaidi nchini Tanzania kwa upande wa tovuti za michezo, ikiwa imefikisha hits milioni tatu (3,074,047) hadi sasa.

Hadi kufikia mwezi huu wa oktoba 2011,  kumekuwa na wastani wa watu elfu kumi wanaotembelea tovuti ya Azam FC kwa mwezi ambapo kurasa 29,000 zimekuwa zikifunguliwa na kufanya wastani wa hits laki tatu kwa mwezi.

Hii ni idadi kubwa sana kwa tovuti ya klabu changa kama Azam FC hasa ikizingatiwa kuwa miezi 12 iliyopita yaani novemba mwaka jana kulikuwa na watembeleaji elfu nne tuu, waliotembelea kurasa 14,000 na hits chini ya laki moja kwa mwezi.

 

Ukiangalia graph ya weblizer utagundua kuwa grafu ya takwimu imeonekana kupanda ukiondoa mwezi may na june, miezi ambayo ligi ilikuwa likizo.

Mtaalamu wa masuala ya tovuti ambaye amehusika kuitengeneza tovuti hii bwana Emmanuel Mnzava anasema kwa uzoefu wake, inawezekana hii ikawa ndiyo tovuti inayotembelewa zaidi nchini (sports website category).

Tayari tumeongeza nafasi kwenye disc (hosting) huku tukiongeza bandwith ili kuweza kukabiliana na ongezeko la watumiaji wa mtandao wetu.

Kibiashara pia tunaweza kusema bidhaa mpya kama azam Cola ambayo SSB imeiingiza sokoni hivi karibuni imekuwa ikinufaika na idadi hii ya watembeleaji wa tovuti ya Azam FC kwani matangazo yake mengi yapo kwenye tovuti ya Azam FC.

Webmaster anawashukuru mashabiki wote mnaotuunga mkono na tunawaahidi kujitahidi kuendelea kuiboresha tovuti yetu ili kuweza kukabiliana na ushindani na kuweza kuwapa taarifa zinazohusu klabu yetu.

Shukrani

Webmaster

Azam FC Website