Mchezaji Joseph Owino ambaye aliichezea simba SC kwa mafanikio makubwa misimu miwili iliyopita na baadaye kupata majeraha ya goti anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India.

Kwa sasa Owino yupo nchini Uganda akiendelea na mazoezi kama alivyopangiwa na daktari wake.

Owino ameiambia tovuti ya Azam FC www.azamfc.co.tz kuwa kwa sasa anajisikia vema na kwa mujibu wa maelekezo ya daktari wake, anapaswa kuanza mazoezi mepesiKutokana na hali hiyo Owino anatarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa  kuendelea na programu ya matibabu chini ya Daktari wa Azam FC. Azam FC inatarajia kumjumuisha Joseph Owino kwenye usajili wa timu yake wakati wa dirisha Dogo hapo December au wakati wa dirisha kubwa July Mwakani kutegemea na Ushauri utakaotolewa na madaktari wa India ambako Owono alikwenda kufanyiwa upasuaji.

Joseph Owino amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili. Uongozi, Benchi la Ufundi na Mashabiki wa Azam FC tunakukaribisha Joseph Owino Azam FC.