Azam FC na Africa Lyon Azam FC leo zitashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa ligi kuu dhidi ya Vodacom.

Mchezo hou utakaochezwa uwanja wa Azam, jijini Dar es Salaam utakuwa wa pili kwa timu zote, Azam FC watacheza wakiwa na pointi tatu walizopata kwa kuifunga Moro United 1-0, huku Lyon watacheza wakiwa na akiba ya pointi moja waliyopata baada ya kutoka sare na Polisi Dodoma katika michezo zao za kwanza kule Dodoma.

Azam FC watacheza mchezo huo na kupumzika kwa muda wa wiki mbili kupisha maandalizi ya timu yaTaifa kwa ajili ya mechi ya marejeano kati ya Taifa Stars na Algeria,mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012.Maandalizi ya mchezo wa kesho yapo vizuri, timu imepumzika baada ya mchezo wa kwanza kwani mwalimu alibaini kuwa wachezaji wake walikuwa na uchovu katika mchezo wa ufunguzi.

Licha ya kuwapa mapumziko ya siku nzima baada ya mchezo wa awali, hapo jana pia mwalimu aliwapumzisha kabisa wachezaji watakaoanza katika mchezo wa leo. Ambapo aliwapiga marufuku kusogelea sehemu ya mazoezi na kuwataka walale vyumbani. Wachezaji hao ni Obren, Shikanda, Waziri, Nafiu, Aggrey, Jabir, Redondo, Sureboy, Bocco, Kipre na Ngasa