Azam FC kesho itafungua rasmi uwanja wake wa Azam Stadium katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu msimu wa 2011-2012 dhidi ya Moro United.

 

Uwanja wa Azam Stadium, upo Chamazi Mbande jijini Dar es Salaam, umekamilika kwa asilimia kubwa isipokuwa jukwaa kuu ambalo pia litakuwa na vyumba vya kubalidilishia nguo wachezaji na baadhi ya ofisi muhimu.

 

Uwanja huo utaanza kutumika kwa maana ya kuchezewa za mechi ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajiwa kuanza rasmi kesho katika viwanja vitano tofauti huku mechi yingine mbili zikichezwa siku ya Jumapili.

 

Ikiwa ni mara yake ya kwanza, uwanja huo pia utatumiwa na timu zingine nne za ligi ambazo zimeuchagua kama uwanja wa nyumbani, timu hizo ni African Lyon, JKT Ruvu, Moro United na Villa Squad.

 

Azam FC itacheza mechi hiyo ikiwa imemaliza ziara yake ya mechi za kirafiki nchini Uganda na Rwanda, kikosi hicho kimecheza mechi nne Uganda, ikafungwa mchezo mmoja sare mbili na kushinda moja, na nchini Rwanda iliifunga Ryon Sports ya nchi hiyo 3-1.

 

Kikosi cha Azam FC kitashuka dimbani hapo kucheza mechi yao ya kwanza ya ligi kuu wakiwa na wachezaji wao mahiri waliosajiliwa kwa ajili ya msimu huu.

 

Wachezaji wote waliosajiliwa wameonyesha uwezo wao wa hali ya juu tangu walipojiunga na kikosi hicho, pamoja na mechi zaidi ya 10 za majaribio walizokuwa wakicheza pamoja.

 

Azam FC itatumia wachezaji waliosajiliwa ambao ni Wahab Yahya, Awud Nafiu, Abdulah Gulam, Said Moradi, Mwadini Ally, Obren Curkovic, Khamis Mcha, Zahor Pazi na Kipre Tchetche.

 

Wachezaji hao wanaungana na wenzao Ibrahim Mwaipopo, Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, Salum Aboubakari, , Haji Nuhu, Daudi Mwasonga, Aggrey Moris, Mrisho Ngassa, Jamal Mnyate,, John Bocco, Malika Ndeule, Ibrahim Shikanda, Himid Mao, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Waziri , na Ramadhna Chombo.

 

Kwa pamoja wachezaji hao watacheza mechi za ligi kuu wakiwa chini ya kocha mkuu Stewart Hall, wasaidizi Kali Ongala, na Iddi Abubakar huku benchi la ufundi likiiwa chachu na meneja Msaidizi Khamis Japhary, Mchua Misuli Mbembe Dunia khamis, madaktari Twalib Mbaraka na Juma Mwanandi Mwankemwa, mtunza vifaa Joseph Yusuf Nzawila na kocha wa timu ya vijana Vivek Nagul