Leo jioni Azam FC itashuka kwenye uwanja wa Amahoro Stadium ambao ndio uwanja mkuu hapa Kigali kukwaana na timu kubwa na yenye mvuto na mashabiki wengi hapa Kigali Ryon Sports.

Azam FC ambao walitua hapa Kigali jana majira ya saa sita mchana, wamefikia katika hoteli ya Sports View ambayo ipo hatua kumi toka uwanja wa Amahoro (mageti ya uwanja na hoteli yanatazamana)

Wachezaji wote wa Azam FC wapo katika hali nzuri isipokuwa Jamal Myate ambaye anasumbuliwa na  homa.

Azam FC jana baada ya kufika ilifanya ziara kwenye kumbukumbu ya mauaji ya Halaiki na baada ya hapo ilielekea kwenye uwanja wa FERWAFA uliopo pembezoni mwa uwanja wa Amahoro kwa ajili ya mazoezi.

Hali ya hewa hapa Kigali ni baridi lakini haionekani kuwasumbua sana wachezaji kutokana na ukweli kuwa wametokea Kampala ambako pia kuna hali ya hewa ya ubaridi.

Kwa mujibu wa kocha mkuu wa timu hii Stewart Hall ambaye amewasiliana na tovuti ya Azam FC kupitia kwa msaidizi wake Kally Ongala, kikosi kitakachoanza leo kinatarajiwa kuwa. 1. Obren/Mwadini 2. Shikanda/Erasto 3. Waziri/Malika, 4. Said Morad/Nafiu 5. Aggrey/Luckson 6. Humud/Himid, 7 Ngasa/Zahoro, 8, Mwaipopo/Jabir, 9. Wahab, 10.Redondo/Sureboy, 11. Kipre/Mcha Viali.

Kabla ya kuja Kigali Azam FC ilicheza mech nne kampala na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo

  1. Azam FC 3-4 Bunamwaya Khamis Mcha 2 Kipre tchetche 1
  2. Azam FC 0-0 SC Villa
  3. Azam FC 3-0 KCC Khamis Mcha 3 Kipre Tchetche 1
  4. Azam FC 1-1 Victors John Bocco 1