Katika ratiba ya ligi kuu ya Vodacom 2011/2012 VPL, Azam FC itafungua pazia la ligi dhidi ya Moro United katika uwanja wa Azam Stadium na siku kumi baada ya ligi kuanza itacheza na Simba SC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Azam FC katika mzunguko wa kwanza itakuwa mwenyeji wa timu za Simba na Yanga, itacheza na Simba, Sept 10, kabla ya kukutana na mabingwa watetezi Yanga, Sep 13, mechi zote zitachezwa uwanja wa Taifa.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limetoa ratiba hiyo ikiwa ni wiki tatu zimesalia kabla ya kuanza kurindima kwa ligi hiyo inayosubiri kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kwa kuwa itakuwa na timu 14 tofauti na ligi iliyopita ilikuwa na timu 12.

Mzunguko wa kwanza utaanza August 20, 2011 na kukamilika Nov 5 mwaka huu, mzunguko wa mwisho wa kumaliza ligi unatarajiwa kuanza 21 Jan, 2012 ,na kukamilika April 1, mwakani.

Azam FC wakitumia uwanja wao wa nyumbani, Azam Stadium uliopo Chamazi Mbane, watacheza mechi ya pili August 23, mwaka huu dhidi ya African Lyon.

Mechi ya nne itakuwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Azam FC wakiwa ugenini dhidi ya JKT Oljoro, Sep 7, Villa Squad wataikaribisha Azam FC, Sep 10, katika uwanja wa Azam FC kabla ya kwenda Tanga, Mkwakwani Stadium kucheza na Coastal Union hiyo itakuwa Sep 21.

Azam FC watakuwa uwanja wa Mlandizi kucheza na maafande wa Ruvu Shootin, Sep 26, watakutana na maafande wengine waliopo ligi kuu mua mrefu JKT Ruvu, Oct 15, katika uwanja wa Azam Stadium, October 21, wataikaribisha Police Dodoma katika uwanja huo.
Mechi zake tatu za kukamilisha mzunguko wa kwanza zitakuwa ugenini, Oct 25, watakuwa Manungu Stadium kucheza na Mtibwa Sugar, wakati Oct 30, watavaana na wakatamiwa wengine Kagera Sugar, katika uwanja wa Kaitaba kabla ya kumaliza mzunguko Nov 5, wakicheza na Toto Africa mchezo utakaochezwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ratiba ya ligi kuu inaonyesha Aug 26-Sep 4, timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ itaweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Algeria, mechi itakayochezwa nchini Tanzania.

Sep 30-Oct13, timu ya taifa itaweka tena kambi kwa ajili ya mechi yake ya mwisho ya kufuzu fainali hizo itakayocheza dhidi ya timu ya taifa ya Morocco, mechi itachezwa nchini Morocco, endapo Stars itafanikiwa kufuzu fainali hizo ratiba ya mzunguko wa pili itasogezwa mbele.