Kikosi cha Azam FC, hapo jana kililazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Kombaini ya majeshi katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam uliopo Chamanzi, jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji John Boko ndiye aliyekuwa wa kwanza kufumania nyavu kutokana na bao lake alilofunga dakika ya 5 baada ya kuchenga mabeki hadi kipa Abdalah Ally ‘Rifat’

Goli la timu ya majeshi mbayo itashiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa yanayohusisha timu za majeshi lilifungwa kupitia kwa kona ya Mohamed Usi ambayo Himid Mao na kipa Mwadin Ally walijichanganya ukapita moja kwa moja.

Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo Stewart Hall, amesema matokeo hayo ni kutokana na kikosi chake kutoka katika mazoezi magumu ya fitinesi, lakini anaimani kikosi chake kitakuwa historia kwenye Ligi kutokana na viwango walivyonavyo nyota wake.

Azam FC, Mwadin/Obren, 2Shikanda/Erasto Nyoni, 3Waziri/Malika 4Nafiu Awudu/Luckson Kakolaki 5Said Murad, 6Abdulhalim Homoud, 7Kipre Tchetche/Waham Yahaya, 8Ibrahim Mwaipopo/Salum Abubakar, 9John Bocco/Zahoro Pazi10 Ramadhani Chombo ‘Redondo’,11Himidy Mao.