Azam FC imeanza maandalizi yake ya msimu wa ligi kuu 2011/12 kwenye kituo chake cha mazoezi Chamazi Complex Mbande jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya jana, kulichezwa mechi kati yao ambapo matokeo yalikuwa 1-1 magoli yakifungwa na Kipre Tchetche na Ghulam Abdulghani  Abdallah.

Katika mechi hiyo wachezaji wapya kama Zahoro Pazi, Waziri Salum, Ghulam Abdallah, Mwadini Ali,  Said Morrad, Kipre Tchetche na Abdulhalim Humud  walitia fora sana na kutoa matumaini makubwa kwenye ligi inayotarajiwa kuanza msimu ujao.

Program ya mazoezi inaonesha kuwa katika siku hizi za mwanzo timu itakuwa ikifanya mazoezi mara sita kwa wiki ambapo mara tatu itakuwa uwanjani na mara tatu itakuwa kwenye Gym.

Wachezaji wanaonekana kuwa na furaha na  wanafurahia mazoezi wanayopewa na waalimu wao.

Wachezaji walioripoti mazoezini hadi sasa ni 18 ambao ni Mwadini  Ally, Waziri Salum, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda , Malika Ndeule, Luckson Kakolaki, Daudi mwaisongwe, Said Morad, Mwaipopo Ibrahim, Ghulam Abdallah, Abdulhalim  Humud, Selembe Selemani kassim, Kipre Herman Tchetche, Omar Mtaki , Jeba Ibrahim Rajab, Mussa John Rooney, Zahoro Pazi na Samih Haji Nunu

Mchezaji Obren Cuckovic anatarajiwa kuwasili weekend hii huku wachezaji toka Ghana wakitarajiwa kutua tarehe 24 alhamisi ijayo ambapo wataungana mazoezini  na wenzao mara moja huku wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa Taifa Stars wakipewa likizo hadi Juni 27 na wale waliokuwa na timu ya U23 wakitakiwa kuripoti mazoezini Juni 29.