Kuimarisha benchi la ufundi, walimu wawili wa Azam FC wanatarajiwa kupata mafunzo ya awali ya ukocha katika mji wa Birmingham mwishoni mwa mwezi huu.

 

Makocha hao ambao watasomea kozi tofauti Kali Ongala atakayechukua mafunzo ya ukocha wa kawaida wakati Iddi Aboubakar Machumu atachukua mafunzo ya ukocha wa magolikipa.

 

Makocha hao wawili wote wakiwa ni wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa nyakati tofauti, watapata mafunzo hayo ya wiki mbili ikiwa ni sehemu ya kuimarisha benchi la ufundi la timu hiyo.

 

Mkamu Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed amesema makocha hao wataondoka nchini siku chache kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo yatakayofanyika katika chuo cha Birmingham Country For Development Scheme Ltd.

 

Azam FC inakuwa klabu ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kupeleka na kugharamia makocha kusomea kozi hiyo.