Siku chache baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Tanzania, VPL, Timu ya Azam FC ambayo imeshika nafasi ya tatu, imeanza harakati za kusajili wachezaji watakaotumika msimu ujao wa 2011/2012.

Azam FC imeanza hatua hiyo mapema ili kuepusha vikumbo vya kugombania wachezaji dakika za lala salama.

Hali hii ya kufanya usajili mapema itasaidia kuwaweka sawa wachezaji wote kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ambao Azam FC imepanga kuvuka hatua ya tatu na kutwaa ubingwa.

Hadi leo Azam FC imesajili adadi ya wachezaji 21, wapya saba na kuongeza mikataba wachezaji 14, wachezaji wapya waliosajiliwa  ni pamoja na golikipa Obren Cuckovic kutoka nchini Serbia na golikipa Mwadini Ali Mwadini kutoka Mafunzo ya Zanzibar.

Wachezaji wengine walioingia mkataba kusaidia klabu hiyo ni Waziri Salum Omar kutoka Mafunzo ya Zanzibar,  Ghulam Abdallah kutoka timu ya Chuoni Zanzibar, kiungo Abdulhalim Humud aliyekuwa akiichezea Simba SC ya Dar es Salaam, Zahor Pazi aliyetoka klabu ya African Lyon na mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu Khamis Mcha Viali kutoka timu ya Zanzibar Ocean View na timu ya taifa ya Zanzibar Heroes.Mbali na wachezaji hao wapya Azam FC imempandisha golikipa Daudi Mwasongwe kutoka timu ya Azam Academy na kuendelea kuwapa nafasi wachezaji chipukizi wa klabu hiyo ambao ni Himid Mao Mkami, Salum Aboubakar na Jamal Mnyate.


Wengine wameendelea kufunga pingu na Azam FC katika msimu ujao ambao ni nahodha Mkenya Ibrahim Shikanda na msaidizi wake Aggrey Moris, mabeki Malika Ndeule, Lackson Kakolaki na Erasto Nyoni, viungo ni Ibrahim Mwaipopo, Seleman Kasim Selembe, Kalimangonga Ongala, Jamal Mnyate na Mrisho Ngassa wakati Mshambuliaji pekee aliyebakishwa kikosini ni John Bocco.

Hadi sasa Azam FC imebakisha nafasi tatu za kusajili ambazo ni beki wa kati na mshambuliaji toka nje ya nchi na beki mwingine wa kati ambaye ni wa humuhumu nchini.

Hadi sasa zimebaki nafasi mbili tuu za kujazia ambazo zitajazwa na wachezaji kutoka Ghana ambao ni beki wa kati na Mshambualia wa kati.

Kikosi kamili cha Azam FC hadi sasa ni

 

Makipa

 1. Mwadini Ally Mwadini

 2. Obren Cuckovic

 3. Daudi Mwasongwe


Walinzi wa Pembeni

 1. Ibrahim Shikanda

 2. Malika Ndeule

 3. Waziri Omar

 4. Erasto Nyoni

Walinzi wa Kati

 1. Aggrey Ambross
 
 

 2. Luckson kakolaki

 3. Said Morrad
 4. Beki toka Ghana

Viungo

 1. Ibrahim Mwaipopo
 2. Salum Abubakar 

 3. Gulam Abdallah

 4. Himid Mao Mkami

 5. Ramadhani Chombo

 6. Abdulhalim Humud 

 7. Jabir Aziz Stima (ana ruhusa ya klabu kwenda Norway)

Washambuliaji  wa pembeni

 1. Mrisho Ngasa

 2. Jamal Mnyate

 3. Khamis Mcha 

 4. Suleimani Kassim
 5. Kipre Herman Tchetche

 

Washambuliaji wa kati

 1. John Bocco

 2. Zahoro Pazzi

 3. Mshambuliaji toka Ghana