Yanga SC jana katika uwanja wa uhuru ilifanikiwa kuifunga Azam FC 2-1 katika mchezo mkali uliokuwa ukisubiriwa na wengi wa ligi kuu Tanzania Bara.

Azam FC ambayo kwa takribani wiki tatu imekuwa ikifanya mazoezi na wachezaji pungufu kufuatia wengi wao kuwa na timu za taifa iliathiriwa sana na majeruhi ambapo wachezaji muhimu kama Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar na Jamal Mnyate wakikosekana kabisa uwanjani huku Himid Mao akilazimika kucheza huku akiwa na majeruhi.

Mchezo wa jana ulikuwa wa kufa na kupona na kwa matokeo ya kufungwa, Azam FC imehitimisha safari yake ya kusaka moja ya nafasi za kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

Kwa masikitiko makubwa tunawapa pole mashaki wetu wote ambao wameumizwa sana na matokeo ya jana na tunawaahidi kufanya usajili wa nguvu kufidia mapungufu yaliyojitokeza msimu huu ili mwakani tuwe bora zaidi.

Dhamira yetu msimu ujao ni kutwaa ubingwa.