Pichani juu, Kocha mkuu wa timu ya Azam FC Stewart Hall akiteta na wachezaji Abdi Kassim Baby na Nadir Haroub Canavaro wa Yanga, Stewart alikuwa kocha wa Zanzibar kabla ya kutua Azam FC na Baby na Kanavaro ni Manahodha wa Zanzibar.

Kesho jumatano tarehe 30 march 2011 katika uwanja wa Uhuru Azam FC na Yanga SC zitamaliza ubishi wa nani ataungana na Yanga kukwea pipa na kucheza mashindano ya Afrika

Kambi ya Azam FC ipo katika hali nzuri sana ukiondoa Ibrahim Mwaipopo ambaye anasumbuliwa na maumivu ya goti, wachezaji wengine wote wapo katika afya nzuri na wanaendelea na maandalizi ya mpambano huo kwenye kituo chetu kilichopitishwa na fifa. Mbande Complex

Kocha mkuu wa Azam FC amelazimika kusogeza jioni mazoezi ya leo asubuhi ili aweze kufanya mazoezi ya mwisho na wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa ya vijana –U23.

Azam FC ina pointi 37 na Yanga SC ina pointi 40, endapo Yanga itaifunga Azam FC basi itahitaji pointi moja tuu kuweza kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika. Na kwa Azam FC endapo itashinda mchezo wa kesho itakuwa imefikisha pointi 40 kama Yanga lakini ikiizidi Yanga uwiano wa magoli na Azam FC itahitajika kumalizia mechi mbili za mwisho kwa ushindi ili nayo iweze kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika.

Mhariri wa Mtandao wa Azam FC, wapigapicha na waandishi wake wote tunaitakia kila la heri Azam FC iweze kushinda mchezo wake wa kesho.