Malika na mashuti ya mbali.

Mchezaji Malika Ndeule juzi asubuhi alikuwa kinara wa mazoezi ya timu ya Azam FC kwa kuweza kufunga idadi ya magoli zaidi ya 15, katika mazoezi ya kikosi hicho yanayofanyika kila siku asubuhi katika uwanja wa klabu hiyo uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Malika amefunga magoli yote kwa mashuti ya umbali mrefu na kuwaa makipa wawili chipukizi wa kikosi hicho Daudi Mwasongo na Wandu Willium waliobadilisha katika vipindi tofauti.

Wakifanya mazoezi chini ya kocha msaidizi Kally Ongala wachezaji waliohudhuria mazoezi walionekana kufurahia mazoezi hayo kwa kucheza vizuri huku wakifata maelekezo ya kocha huyo.

Mchezaji Salum Aboubakar yeye ameendelea kuongeza uwezo wa kumiliki na kuchezea mpira, aliweza kuwatesa wachezaji wenzake bila kuangalia maumbile yao , kwani wenzake wana miili ilijongeka kuliko yeye.

Mbali na hayo wachezaji wamefanya mazoezi kama kawaida kwa kufuata mfumo wa kocha mpya Stewart Hall wa 4-3-3.

Mchezaji Cosmas Lewis kutoka kikosi cha Azam Academy ameendelea kufanya mazoezi na timu hiyo na kuonyesha uwezo mkumbwa akiwa kama mshambuliaji, aliweza kufunga goli zuri katika mazoezi hayo kuliko wachezaji wengine.

Golikipa Vladimir Niyonkuru aliendelea kuonyesha umahiri wake wa kuwa kipa namba moja wa kikosi hicho kwa kuokoa mashuti yaliyokuwa yakipigwa na wachezaji wenzao na kuwa golikipa aliyeruhusu magoli machache kuliko wote kwa kufungwa magoli sita katika mchezo minne.

Timu za leo zilikuwa na wachezaji saba kila moja, na kucheza nusu uwanja, timu ya kwanza ilikuwa na wachezaji Vladimir Niyonkuru/Wandu Willium, Erasto Nyoni, Luckson Kakolaki, Cosmas Lwis, Malika Ndeule na Mutesa Mafisango.

Wakati timu nyingine iliundwa na Daudi Willium/Jackson Chove, Sino Augustino, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Tumba Swed, Mau Bofu, Ally Manzi na Ibrahim Mwaipopo.

Kocha msaidizi Kally Ongala alisema timu inaendelea kufanya vizuri wakati wakisubiri wachezaji waliitwa Taifa Stars kurejea ili kuendelea na maandalizi zaidi ya mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon.

“Tunaendelea vizuri wachezaji wamebadilika na kucheza kwa malengo, hivyo wengine watakaporudi kutoka Taifa Stars tutaendelea na maandalizi zaidi.”alisema Kally.

Kocha Stewart aliyekuwa nchini Uingereza anatarajiwa kurejea leo hii kuendelea na program yake.

 

Nyoni: kutumia uwanja wetu imetusaidia na kutufanya tujiachie zaidi

Beki mahiri wa kikosi cha Azam FC, Erasto Nyoni amesema kutumia uwanja wake wa nyumbani kufanyia mazoezi kumeleta mabadiliko kwa timu kutokana na kufanya mazoezi kwa muda.

Nyoni amesema tofauti na ilipokuwa mwanzo katka viwanja vya kukodi, timu ilikuwa inalazimika kumaliza mazoezi mapema ili kupisha taratibu nyingine za uwanja, lakini sasa wanafanya mazoezi kwa muda muafaka.

“tumefarijika kuhamia katika uwanja wetu, sasa tunafanya mazoezi na kukamilisha program iliyopangwa, wachezaji wanapata muda mrefu wa kufanya mazoezi na kupumzika hali inayopelekea timu yetu kuwa nzuri zaidi.”amesema Nyoni.

Nyoni anaamini kuwa kuwepo kuendelea kuutumia uwanja huo kwa maandalizi na mazoezi utaimarisha zaidi kikosi hichi na kuleta upinzani zaidi katika michezo yake ya ligi kuu.

“uwanja wetu ni wa kisasa unakaribia kuwa kama Uwanja wa Uhuru na Karume lakini nyasi bandia za huku ni nyembamba na laini, unatusaidia kwa kuwa unafanana na uwanja tunaochezea mechi za ligi kuu.”amesema Nyoni.

Anaongeza kuwa pindi wanapokuwa uwanjani hakuna wakuwasimamia kuhusu muda, wanafanya mazoezi kwa muda wanaotaka na kumaliza muda wowote wanaotaka tofauti awali ambapo wanapewa muda usiozidi masaa mawili.